|
PSG sasa wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Di Maria wakati ambapo Manchester United wakisua sua |
Paris Saint-Germain imekuwa yenye nafasi kubwa kuliko nyingine zote ambazo zinamfukuzia winga wa Real Madrid Angel Di Maria.
Winga huyo anaonekana hana nafasi tena ndani ya viunga vya Bernabeu
baada ya Real kuonekana kumtaka zaidi kiungo mchezeshaji raia wa Colombia James Rodriguez kuwa ndiye mchezaji namba moja katika mawindo yao.
Di Maria aliisaidia Real Madrid kushinda 'la decima'
PSG kwasasa wanaamini kuwa wako mbele zaidi katika harakati za kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 26 Di Maria, ambaye mkataba wake na Madrid una muda wa miaka minne.
Di Maria anawaniwa pia na Manchester United huku Madrid wenyewe wakimthaminisha kwa karibu pauni milioni £50.
Taarifa zinasema kuwa United bado haijaweka rasmi mezani mpango wa kumnasa Di Maria ingawa kuonekana kuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment