Nyota bora wa zamani wa dunia Ronaldo de Lima |
Aliyekuwa mchezaji bora duniani Ronaldo Luís Nazário de
Lima, ameikosoa timu ya taifa ya Brazil kwa kusema bado kuna wachezaji
wanacheza chini ya kiwango, hali ambayo inamuogopesha katika kipindi hiki cha
michezo ya hatua ya mtoano inayoendelea kwenye michuano ya kombe la dunia.
Ronaldo, ambaye alikuwa mchezaji bora duniani kwa vipindi
vitatatu tofauti na hiyo ilikuwa ni mwaka 1996, 1997 pamoja na 2002 amesema
mpaka sasa anaona kuna mapungufu makubwa katika safu ya ushambuliaji ambayo
haijatumikiwa ipasavyo.
Amesema mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar da Silva
Santos Júnior ndiye mchezaji pekee anayempa matumaini kutokana na mchezo mzuri
anaoendelea kuuonyesha, lakini kwa washambuliaji wengine kama Jo na Fred bado
kuna mashaka kwake.
Katika hatua nyingine de Lima, amesema ana imani kubwa na
kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Luis Philipe Scolari atafanya mabadiliko
kuelekea katika mchezo wa hii leo ambapo The Canarinho watakuwa wakicheza
mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Colombia.
Mchezo mwingine wa hatua ya robo fainali ya kombe la dunia
utakaochezwa hii leo ni kati ya timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya mabingwa wa
soka wa dunia mwaka 1998 timu ya taifa ya Ufaransa.
No comments:
Post a Comment