Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salum Madadi kuendesha semina ya kupinga rushwa katika soka |
Shirikisho la soka nchini TFF linajipanga kuendesha semina maalum
kwa maafisa wa klabu za ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza ambayo italenga
kampeni dhidi ya upangaji matokeo.
Mkurugenzi wa michezo wa shirikisho hilo Salum Madadi
amesema baada ya maafisa taasisi inayoendesha kampeni dhidi ya upangaji matokeo
kutoka nchini Uingereza kutoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana
pamoja na waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita, hatua inayofuata
itawahusu viongozi wa klabu za ligi kuu na daraja la kwanza.
Madadi amesema lengo kubwa la kuwahusisha viongozi wa klabu
za ligi kuu na daraja la kwanza ni kutaka kutoa elimua mbayo itakuwa tahadhari
kwa viongozi hao ambao kwa asilimia kubwa huenda wakawa chanzo cha kujihusisha
suala la upangaji wa matokeo.
Hata hivyo Salum Madadi amesema kamepeni dhidi ya upangaji
wa matokeo haitoishia kwa viongozi wa klabu za ligi kuu pamoja na daraja la
kwanza, bali wataifikisha hadi kwa vijana wanaochipukia kwenye medani wa soka.
No comments:
Post a Comment