KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 6, 2014

Bayern Munich wakubali kumsajili Jese Manuel 'Pepe' Reina Paez

Pepe Reina
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, wamekubali dili la kumsajili mlinda mlango kutoka nchini Hispania na klabu ya Liverpool José Manuel "Pepe" Reina Páez.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Allianze Arena Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha ukamilifu wa dili hilo kupitia tovuti ya The Bavarians kwa kusisitiza Reina atajiunga nao baada ya kukamilisha zoezi la kupimwa afya. Rummenigge, amesema wana matumaini makubwa na kipa huyo mwenye umri wa miaka 31, kutokana na kiwango chake kizuri hivyo wanaamini atasaidiana vyema na mlinda mlango wao namba moja Manuel Neuer.
Amesema kusajiliwa kwake hakumaanishi anakwemnda kuwa kipa chaguo la pili, bali wanatarajia kuona kujituma kwa Manuel Neuer na kuleta ushindani wa kuwania nafasi ya kukaa langoni.
Msimu uliopita Pepe Reina alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli ya mjini Naples nchini Italia, baada ya meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers kumsajili Simon Mignolet.
Wakati huo huo meneja wa FC Bayern Munich Josep Pep Guardiola Isala amekanusha uvumi wa kutaka kumruhusu beki Jerome Boateng kujiunga na FC Barcelona.