KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 6, 2014

FC Barcelona wamewasilisha ofa ya paund million kumi kwa ajili ya Thomas Vermaelen


FC Barcelona wamewasilisha ofa ya paund million kumi huko kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal, ambapo wanaamini ofa hiyo inatosha katika harakati zao za kutaka kumsajili beki wa kati kutoka nchini Ubelgiji Thomas Vermaelen.

Barcelona wametuma ofa hiyo kwa kutumia nafasi iliyotangazwa na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger mwishoni mwa juma lililopita ya kutoa ruhusa ya kuondoka kwa Vermaelen licha ya kukiri bado anatamani aendelee kubaki kikosini kwake.

Sababu kubwa ya beki huyo mwenye umri wa miaka 28, kufunguliwa milango huko Ashburton Grove ni uwajibikaji wake wa kila siku ambao unaonekana kushuka kutokana na majeraha ya mara kwa mara yanayomkabili.

Wenger amemuweka sokoni Vermaelen, huku akimini safu yake ya ulinzi itakua sawa sawa wakati wa msimu wa ligi ya nchini Uingereza pamoja na michuano ya kimataifa kwa mwaka 2014-15.

Hata hivyo FC Barcelona huenda wakapata upinzani katika harakati za kumsajili Thomas Vermaelen, kufuatia mikakati inayopangwa na uongozi wa klabu ya Man Utd ya kutaka kumbakisha beki huyo nchini Uingereza.

Barca wanajipanga kumsajili Thomas Vermaelen kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Carles Puyol, aliyetangaza kustahafu soka msimu uliopita kutokana na shinikizo la majeraha yaliyomkabili mara kwa mara.