KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 24, 2014

CAF wanataka adhabu kali kutolewa kwa aliyehusika na kifo cha Albert Ebosse nchini Algeria

Rais wa Caf Issa Hayatou
Shirikisho la soka barani Afrika limetaka tatu ya kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa kufuatia kifo cha mshambuliaji wa timu ya JS Kabylie Albert Ebosse. 

Mkameroon huyo amefariki dunia akiwa hospitali kufuatia kupigwa na jiwe lililorushwa kutoka jukwaani katika mchezo wa ligi ya nchini Algeria. 

"Soka la Afrika haliwezi kuwa uwanja wa kuvujisha damu kunako fanywa na wahuni" Amesema Rais wa Caf Issa Hayatou.

Ameongeza kwa kusema 
"Tunategemea adhabu kali kutolewa dhidi ya kitendo hiki cha vurugu zisizovumilika." 
 
Ebosee mwenye umri wa miaka 24, alipigwa kichwani na jiwe lililorushwa kutoka jukwaani na mashabiki wakati timu zikitoka uwanjani baada ya mchezo kukamilika.