KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 24, 2014

Carlo Ancelotti amewaka maini Arsenal kuhusu Sami Khedira

Matumaini ya Arsenal ya kumsajili Sami Khedira kipindi huki cha usajili yamegonga mwamba kufuatia kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuthibtisha kuwa kiungo huyo ataendelea kusalia nchini Hispania.

Washika mitutu walikuwa wakiaminika kuwa katika maandalizi ya uhamisho wa Mjerumani huyo kwa pauni milioni 12 wiki hii kufuatia Ancelotti hivi karibuni kudai kuwa kiungo huyo alikuwa huru kusaka muelekeo mpya.

Lakini kocha huyo Mtaliano mwenye umri wa miaka 55 sasa anakanusha kutaka kumuuza Khedira kipindi hiki.

Ananukuliwa akisema
‘Khedira anafuraha hapa, na atasalia hapa, mambo yamewekwa sawa na sasa anaendelea hapaReal Madrid,’ Amesema Ancelotti.