KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 24, 2014

Klabu bingwa Afrika Al- Ahly ya Misri yatinga nusu fainali sambamba na Sewe Sport ya Ivory Coast

Kigogo cha Misri , Al-Ahly na Sewe Sport ya Ivory Coast wamefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika katika siku ya mwisho ya michezo ya kundi B iliyofanyika hapo jana.

Sare ya bila mabao dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mjini ilitosha kuwavusha mashetani wekundu wa Misri katika hatua ya hiyo ilhali Sewe Sport wakitinga baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Zambia Nkana mchezo uliopigwa mjini Abidjan.

Ahly wenye rekodi ya kushinda mara nane taji la vilabu Afrika wamemaliza katika kundi wakiwa na alama tisa kama ilivyo kwa Sewe Sport, lakini wakiwa juu ya kutokana na matokeo ya kufungana wenyewe kwa wenyewe.

Ahly atakutana na mshindi wa pili wa kundi A katika nusu fainali wakati Sewe Sport akimsubiri mshindi wa kundi hilo la A.

Bingwa wa Cameroon Coton Sport tayari amekwisha kufuzu kutoka katika kundi A huku nafasi ya pili ikisubiri matokeo ya mchezo kati ya AC Leopards ya Congo na AS Real ya Mali.