KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 25, 2014

Baada ya Liverpool kuelekea kwa Mario Balotelli sasa Samuel Eto'o kujiunga na Everton

Samwel Eto'o kuelekea Goodson Park kiangazi hii
Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o sasa huenda akajiunga na kikosi cha Roberto Martinez Everton baada ya Liverpool kuondoa nia ya kusajili.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid, Barcelona, Inter Milan na Chelsea striker yuko huru kufuatia kukamilisha mkataba wake wa mwaka mmoja Stamford Bridge mapema kiangazi.

Akiwa na heshima ya kushinda tuzo ya klabu bingwa Ulaya,Eto’o amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa kiangazi hii lakini taarifa za hivi punde zinaonekana wazi kuwa Everton maarufu kama Toffees wameshindwa mbio za kupata huduma yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka The 33 amehifadhi rekodi nzuri ya kufunga zaidi ya magoli 300 na Martinez anataka mtu wa kutumainiwa nyuma ya mshambuliaji wake Romelu Lukaku.

Arouna Kone amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi na bado ataendelea kukosekana ilhali Steven Naismith akiwa ndio mshambuliaji namba mbili.

Eto’o atalazimika kupunguza kiasi cha malipo anayotaka cha pauni £130,000 kwa wiki endapo atakabidhiwa mkataba wa miaka miwili ambao inaonekana ni kama Everton imefanya usajili kwa fedha fedha nyingi msimu huu wa uhamisho.