KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 24, 2014

Mpango wa Angel Di Maria kutua Manchester United waingia shubiri

Angel Di Maria kujiunga na United ni kizungumkuti
Manchester United imeshikwa na kigagaziko kufuatia klabu ya Real Madrid kutaka kuvunja rekodi ya kuuza wachezaji Uingereza kwa pauni milioni £75 kwa ajili ya usajili wa Angel Di Maria.

Winga huyo wa kimataifa wa Argentina amewaweka katika hali ya utayari mabingwa ywa Ulaya Real Madrid na muelekeo ukiwa ni Old Trafford na taarifa zikisema kuwa amenza kutoa mkono wa kwakheri kwa wachezaji wenzake tangu Jumamosi ya jana.

Manchester United wamekuwa wakipambana kupata saini ya winga huyo lakini taarifa za hivi punde zinasema kuwa Madrid wanataka kuvunja rekodi ya Uingereza ya kuuza wachezaji kwa bei kubwa ambazo zimewashitua United.

Walikuwa wakitegemea thamani ya mpaka pauni milioni £56, sawa na kiasi kilichojadiliwa na wapinzani wao Paris St Germain wiki iliyopita, lakini Madrid wamerejesha nyuma matumaini ya United ya kupata winga huyo wakiweka dau kubwa la ada yake.

Bado mpango huyo haujafa kabisa ikiwa ni wiki nzima imesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa kiasi kutoa matumaini kwa United kuanza mazungumzo upya angalau wapate punguzo ambalo linaweza kukubalika.

Rais wa Madrid Florentino Perez anamuona Di Maria kama ndio jibu la kuimarisha mfuko wa klabu hiyo kiangazi hii, na kwamba kuuzwa kwake kunaweza kukawa chachu ya kumchukua mchezaji Radamel Falcao kutoka katika klabu ya Monaco.

Endapo United watafika bei wanayo itaka, hiyo ina maana kuwa Madrid watakuwa wamepata faida kubwa ikilingalishwa na bei waliyo mnunua kutoka Benfica kwa kiasi cha pauni milioni £20 mwaka 2010.

Rekodi ya sasa ya Uingereza ya kuuzwa kwa wachezaji ghali inashikiliwa na Fernando Torres ya pauni £50 akitokea Chelsea mwaka 2011.