KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 18, 2014

Coastal Union kuwafuata Yanga huko Pemba kwa kambi ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara

Kocha Yusufu Chipo
Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kuondoka mkoani Tanga kesho
kuelekea Visiwani Pemba kwa kutumia usafiri wa Ndege kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza mwezi Septemba 20 mwaka huu.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa timu hiyo itaondoka kesho saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga
wakiwa na msafara wa wachezaji 28 na viongozi sita.

Assenga amesema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kwenye viwanja vya migombani visiwani humo asubuhi na jioni wakiwa na lengo kuu la kuhakikisha wanajiandaa vema na michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara.

Amesema kuwa kati benchi la ufundi litakuwa likiongozwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Yusuph Chippo, Msaidizi wake Benard Mwalala, Kocha wa
Makipa Razack Siwa na daktari wa timu na mtunza vifaa.