KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 18, 2014

Liverpool yamruhusu Tiago Ilori kujiunga na Bordeaux kwa mkopo

Ilori sasa kwa mkopo klabuni Bordeaux
Mlinzi wa Liverpool Tiago Ilori amejiunga na Bordeaux kwa mkopo wa muda mrefu ndani ya msimu.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 21 alisaini kujiunga na kikosi cha kocha Brendan Rodgers mwezi September mwaka jana kabla ya kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Granada mwezi  Januari ambako alicheza michezo tisa katika klabu hiyo ya nchini Hispania.

Ilori, mlinzi wa kimataifa wa Ureno katika kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 amekuwa akihusishwa na kuelekea kwa mkopo  katika klabu ya Borussia Dortmund kabla ya kuelekea Bordeaux.

Kwasasa klabu hiyo imekalia nafasi ya pili katika ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 kufuatia ushindi wa mabao 4-1 Jumapili iliyopita dhidi ya Monaco.