KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 3, 2014

Msumbiji yaichapa Taifa Stars na kupaisha ndoto za kutinga hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika

Taifa Stars ya Tanzania iliyokuwa uwanja wa Zempeto jijini Maputo imeshindwa kutamba mbele ya wenyeji Msumbiji na kuambulia kichapo cha mabao 2-1, na kuyeyusha matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika. Kabla ya mchezo huo Stars ilikuwa ikihitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kuwerza kusonga mbele lakini haiukuwa hivyo na kushuhudia dakika 90 zinakamilika wakiwa nyuma ya mabao 2-1. Msumbiji waliandika bao la uongozi dakika 45 likifungwa na Josimar kabla ya Mbwana Samata kusawazisha kunako dakika ya 77 goli ambalo lilidumu kwa dakika 5 kabla ya msumari wa mwisho kwa wenyeji kushindiliwa na Dominguez kunako dakika ya 83. Matokeo hayo nayairejesha vichwa chini Stars ambayo sasa itakuwa haina la kushindania barani Afrika.