Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa akimtoka Erasto Nyoni wa Azam fc katika mchezo wa ngao ya jamii uliomalika kwa matokeo ya Yanga kushinda bao 3-0 uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. |
Mjini Kila Mtu ni Jaja tu......
Wengine mwisho wao Chalinze....
Hayo ni maneno ya wapenzi wa soka walioshuhudia mchezo wa leo kati ya
Young Africans dhidi ya Azam FC baada ya mbrazil huyo kuonyesha kazi ya
mshambuliaji uwanjani.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka
nchini Brazil Geilson Santos "Jaja" leo amewaonyesha wapenzi wa soka
nchini nini kazi yake uwanjani baada ya kuisadia Young Africans kuibuka
na ushindi wa mabao 3-0 huku yeye akikwamisha mabao mawili safi mchezo
uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele
ya mashabiki wake zaidi ya elfu thelathini waliofurika kuwapa morali
wachezaji, walitulia na kucheza soka tangu mwanzo wa mchezo mpaka
mwisho.
Kocha Mbrazil alianza na mfumo wa 4-5-1 walinzi Juma Abdul
Oscar Joshua, Kelvin Yondani na Nadri Haroub "Canavvaro", mbele yao
wakicheza viungo wa Ulinzi Mbuyu Twite na Said Juma "Makapu" wakisaidiwa
na Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa na mbrazil Jaja akianza mshambuliaji
peke yake.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu zote
kusaka bao la mapema, mipira mirefu ya Mbuyu Twite kwa Mrisho Ngasa
haikuwa na madhara sana langoni mwa timu ya Azam katika dakika 10 za
mwanzo.
Kiungo Said Juma "Makapu" alikosa nafasi ya kuipatia Young
Africans bao la kwanza dakika ya 10 baada ya mpira wa kona uliopigwa na
Niyonzima, huku Nizar Khalfani pia akikosa kuifungia pia timu yake bao
baada ya shuti la faulo alilopiga kutoka mita chache pembeni mwa lango
la Azam.
Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Azam FC
kupitia kwa washambuliaji wake Geilson Santos "Jaja" Mrisho Ngasa na
Nizar Khalfani lakini kutoku makini kulipelekea timu zote kwenda
mapumziko zikiwa sare ya kutofungana.
Kipindi cha pili Young
Africans ilianza kwa kufanya mabadiliko ambapo kocha aliwaingiza Hassan
Dilunga na Saimon Msuva waliochukua nafasi za Said Juma na Nizar
Khalfani hali iliyopelekea kikosi cha mbrazil Maximo kutawala eneo la
kiungo.
Dakika ya 58 Geilson Santos "Jaja" aliwainua vitini
mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Young Africans baada ya
kuipatia timu yake bao la kwanza katikati ya walinzi wawili wa Azam FC
akiitumia vizuri pasi ya Saimon Msuva.
Geilson Santos "Jaja"
dakika ya 66 ya mchezo aliwainua tena vitini washabiki, wapenzi na
wanachama baada ya kufunga bao la pili kwa ufundi wa hali juu, baada ya
kupenyezewa pasi nzuri na kiungo Hassan Dilunga na Jaja kuukota kwa
hatua moja na kisha kumchambua mlinda mlango wa Azam FC Mwandini Ali kwa
kuunyanyua kwa ufundi na kuamsha shangwe na nderemo uwanjani.
Huku
wapenzi wa soka wakidhania mpira umemalizika, Saimon Msuva alimaliza
ndoto za timu ya timu ya Azam kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuipatia
timu yake bao la tatu na ushindi na kuifanya Young Africans kuchukua
Ngao ya Jamii kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake huku Simba wakiwa
wamechukua mara mbili na Mtibwa Sugar mara moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 Azam FC.
Mara
baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mbrazili Marcio Maximo
amesema anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo
yake hali iliyoplekea kucheza soka safi la kuburudisha linaloambatana na
ushindi.
Aidha Maximo amesema
baada ya ushindi wa leo maandaliz ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar
yataanza siku ya jumanne ambapo kwa kesho ametoa mapumziko kwa wachezaji
wote pamoja na benchi la Ufundi.
Mwisho
Maximo amewapongeza vingozi, waachezaji na washabik wa Young Africans
kwa sapoti wanayoitoa kwa timu na kuomba wajitokeze kwa wingi pia mjin
Morogoro mwishoni mwa wiki katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Young
Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir
Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite, 7.Said Juma
"Makapu"/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Hamis Kizza, 9.Geilson
Santos "Jaja"/Hussein Javu, 10.Mrisho Ngasa/Omega Seme, 11.Nizar
Khalfani/Saimon Msuva/
Azam
FC: 1.Mwadini Ali, 2.Shomari Kapombe, 3.Erasto Nyoni/Gadiel Michael,
4.David Mwantika, 5.Agrrey Morrsi, 6.Kipre Balou, 7.Himid Mao/Kelvin
Friday, 8.Salum Abubakar, 9.Didier Kavumbag, 10.Kipre Tchetche/Ismail
Diara, 11.Leonel st.Pres/Khamis Mcha
No comments:
Post a Comment