KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 15, 2014

Daley Blind anasema Sir Bobby Charlton ni mtu tofauti ukimlinganisha na Sir Alex Furguson ndani ya ngome kongwe Old Trafford

Mkongwe wa Manchester United Sir Bobby Charlton (kulia) akiwa na meneja wa United Louis van Gaal
Nyota mpya wa Manchester United Daley Blind ameweka wazi juu ya kuvutiwa na mkongwe wa ngome kongwe 'Old Trafford' Sir Bobby Charlton ambaye bado anatembelea kikosi cha Louis van Gaal katika chumba cha kubadilishia nguo kila baada ya mchezo mmoja tofauti na Sir Alex Furguson.
Mengi yemekuwa yakifanyika na kusemwa katika siku za karibuni kati ya meneja wa zamani Sir Alex Ferguson na bosi mpya wa Old Trafford na Luis Van Gaal, ambapo Ferguson ametanabaisha wazi kuwa ataendelea kujiweka mbali na mduchi Van Gaal.
Lakini inaonekana Sir Bobby anaendelea kutumia uwepo wake kujaribu kuwapa nguvu wachezaji wakati ambapo Van Gaal akijitahidi kujipanga zaidi katika klabu hiyo mpya
Charlton scores one goal of a glorious career against Manchester City at Maine Road in November 1969
Charlton akifunga moja kati ya magoli yake mazuri wakati wa uchezaji wake dhidi ya Manchester City huko Maine Road Novemba 1969
Sir Alex Ferguson is, unlike Charlton, keeping his distance from the players by watching from the stands
Sir Alex Ferguson si kama Charlton, amejiweka mbali na wachezaji kwa kuangalia mchezo wa timu hiyo akiwa jukwaani.

Blind aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya Ajax amesema 'ni vizuri kuona utamaduni unadumishwa na kuwa imara katika klabu ya United, kwa mfano ziara ya Bobby Charlton ndani ya vyumba vya kubadilishia ngu kila baada ya mchezo.
'Sir Bobby haongei sana, lakini anakuwepo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo akiwa amesimama.
'anaishi kama mkongwe wa klabu na ina maana kwetu anapokuja.'
Sir Bobby ndio ametoka katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 77 na ameendelea kuwa mtu muhimu United'.
Hivi karibuni alikimbizwa hospitali baada ya kupatwa na mshituko wa tumbo wakati akicheza mchezo wa gofu nchini Scotland lakini sasa amerejea katika shughuli zake za kila siku ndani ya klabu.