KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 15, 2014

Hivi ni kweli Messi na Ronaldo wanategemeana licha ya kwamba hawachezi timu moja? Soma hapa....

Ronaldo na Messi wanategemeana katika kufunga magoli

Nyota wa zamani wa vilabu vya Real Madrid na Barcelona Michael Laudrup anaamini kuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanategemeana katika kujiimarisha.
Nyota hao wawili wamekuwa katika viwango vya juu vya kimchezo na katika hali ya kiupinzani baina yao karibu muongo mmoja uliopita, wakishinda tunzo ya Ballon d'Or kwa kuppkezana tangu mwaka 2008 na kufunga idadi kubwa ya mabao kupita 50 katika mashindano yoye kila msimu.
Laudrup, ambaye aliitumikia kwa kipindi cha miaka mitano Camp Nou kabla ya kuelekea Santiago Bernabeu mwaka 1994, anaamini wawili hao watakumbukwa sana hata baada ya ustaafu wao wa soka kama wachezaji wenye mafanikio zaidi kuwahi kutokea katika mchezo wa mpira wa miguu.
Amekaririwa akisema "Nadhani wanategemeana,"Alikuwa akiongea na EFE.
"Kama mmoja akifunga 'hat-trick', mwingine anapambana kulipiza hiyo. ni watu wawili walio katika kiwango cha juu sana na mafanikio, si tu katika kizazi hiki ni hata baada ya miaka 30 ijayo watazungumziwa sana na mjadala utakuwa ni nani kati ya Messi, Cristiano, Maradona au amewahi kutokea kuwa mchezaji mkubwa zaidi ya mwingine katika kipindi chote."