KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 2, 2014

Dr Damas Ndumbaru: Ubabe wa Jamali Malinzi kwa bodi ya ligi na vilabu, utasimamisha ligi kuu na kuelekea FIFA

Mwanasheria wa Vilabu Dr Damas Ndumbaru anasema Malinzi atasimamisha ligi kuu kwani vilabu havikubaliani na ubabe wake
Muda mfupi baada ya Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamali Emily Malinzi kutangaza kuvibana vilabu vya ligi kuu kuchangia mapato yao kwa asilimia tano ili kuchangia miradi mbalimbali iliyo anzishwa na shirikisho la soka nchini, vilabu vya ligi kuu kupitia kwa mwanasheria wao Dr Damas Ndumbaru vimetishia kugomea kuendelea na ligi kuu ya soka inayoendelea hivi sasa na kumtaka Malinzi kuachana na agizo hilo ambalo linaonekana lina lengo la kuvinyonya zaidi vilabu.

Akiongea katika mazunguzo maalum na mtandao huu wa Rockersports, Ndumbaru amesema tayari amezungumza na wateja wake ambao ni vilabu na wamekubaliana mambo kadhaa ikiwemo kuachana na ligi kuu pamoja na kuelekea shirikisho la soka duniani FIFA endapo Rais Malinzi atang'ang'nia msimamo huo.
Rockersports audio
Msikilize mwanasheria wa vilabu Dr Damas Ndumbaru akipingana na Malinzi

No comments:

Post a Comment