KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 17, 2014

Premier League: Chelsea wataweza kupanua mwanya wa alama kileleni dhidi ya Palace kesho?

Chelsea wataelekea kwa wapinzani wao jijini London Crystal Palace Jumamosi wakilenga kupanua mwanya wa alama tano walioweka kileleni mwa Ligi ya Premia huku ligi ikirejelewa baada ya mapumziko ya kimataifa.
Palace walishangaza Chelsea, na klabu nyingine katika ligi, kwa kushinda dhidi ya Chelsea msimu uliopita na nahodha wa Blues John Terry amepuuzilia mbali madai kwamba tayari mshindi wa ligi msimu huu amejulikana.
“Ni wazi (kwamba kinyang’anyiro cha ligi) hakijaisha,” amesema Mourinho.
“Klabu nyingine zimejipata katika nafasi kama hii. Ni vyema kuongoza lakini ukiwa juu, kila mtu hutaka kukuangusha.
“Hilo ndilo jambo zuri kuhusu Ligi ya Premia na ndio maana kila mtu huipenda. Timu zinalenga kutushambulia kwa sababu tuko juu na twacheza vyema.”
Mabingwa watetezi Manchester City, walio wa pili kwa sasa, watakuwa nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspur na kiungo wa kati anayeichezea City kwa mkopo Frank Lampard amewaambia wachezaji wenzake wajihadhari dhidi ya Spur ambao wameanza kuamka.
“Huenda wanapitia kipindi cha mpito lakini nilifurahishwa sana na meneja wao (Mauricio Pochettino) alipokuwa Southampton na ikiwa anaweza kufanya hayo Tottenham, ambao bila shaka wana vipaji kwenye kikosi chao, watafana. Ni timu nzuri sana.”

No comments:

Post a Comment