Karim Bellarabi |
Mshambuliaji wa kulia wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi amechaguliwa
katika timu ya taifa ya Ujerumani. Mchezo mzuri wa Max Kruse msimu huu
pia umempa tikiti ya kujumuishwa katika kikosi cha taifa.
Bellarabi ameitwa katika timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza
kwa ajili ya mechi mbili za mwezi huu dhidi ya Poland na Jamhuri ya
Ireland.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu
katika ligi ya taifa baada ya kumaliza msimu uliopita katika klabu
iliyoshushwa ngazi ya Eintracht Braunschweig kwa mkataba wa mkopo. Chini
ya kocha mpya Rodger Schmidt, Bellarabi amefunga magoli mawili katika
mechi zake sita za kwanza, na kuwaandalia wenzake magoli matatu ya
Leverkusen kwenye ligi ya Ujerumani.
Max Kruse wa Borussia Mönchengladbach anarejea baada ya kuwa nje mechi
kadhaa kutokana na jeraha. Bastian Schweinsteiger, Sami Khedira, Marco
Reus na Mario Gomez wamewachwa nje ya mechi hizo mbili ambazo zitachezwa
Octoba 11 na 14.
Kikosi kamili cha Ujerumani:
Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover)
Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Borussia
Dortmund), Matthias Ginter (Borussia Dortmund), Mats Hummels (Borussia
Dortmund), Shrokdan Mustafi (Valencia), Antonio Rüdiger (Stuttgart),
Sebastian Rudy (Hoffenheim)
Viungo: Karim Bellarabi (Leverkusen), Julian Draxler (Schalke),
Toni Kroos (Real Madrid), Christoph Kramer (Gladbach), Thomas Müller
(Bayern Munich), Mesut Özil (Arsenal), Lukas Podolski (Arsenal), Andre
Schürrle (Chelsea)
Washambuliaji: Mario Götze (Bayern Munich), Max Kruse (Gladbach)
No comments:
Post a Comment