![]() |
Alisher Usmanov bilionea mmiliki wa hisa Arsenal |
Mwanahisa wa
pili kwa ukubwa wa hisa yake katika klabu ya Arsenal Alisher Usmanov amekosoa
uendeshwaji wa klabu hiyo baada ya Robin van Persie kutangaza kuwa hana mpango
wa kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo.
bionea huyo
raia wa Uzbektan ameitumia barua yenye maneno makali bodi ya klabu hiyo akiwashutumu
kwa kukosekana uwekezaji ndani ya klabu hiyo.
"bado
kwa mara nyingine tunakabiliwa na kupoteza wachezaji wetu wa ukweli mwenyewe
akitumia neno ‘true marquee’ kwasababu hatuwezi kuwapa hali ya kujiamini kwao
kuwa tunaweza kushinda mataji.
“kama klabu
kubwa tuanapaswa kwa dhati kabisa kulingana au kushinda offer za klabu nyingine kwa
kujaribu kuwapa mazingira mazuri wachezaji wetu wazuri na kuwajengea
mustakabali mzuri wa baadaye”
Kroenke alijaribu
kutaka kukamilisha umiliki wa hisa katika klabu hiyo mwaka 2011 lakini Usmanov mwenye umri wa miaka 58 alisisitiza
kutokuwa tayari kuuza hisa yake hiyo.
Mshambuliani
Van Persie mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika maktaba
wake hapo jana alitanabaisha kuwa yeye, meneja Arsene Wenger na mtendaji wa
klabu Gazidis walishindwa kukubaliana jinsi ambavyo klabu itaendelea katika
siku za usoni.
No comments:
Post a Comment