![]() |
Makamu mwenyekiti Geofrey Nyange Kaburu akionyesha waandishi wa habari mkataba wa Okwi |
Uongozi
wa Klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam imesema mshambuliaji EMMANUEL OKWI bado
ni mchezaji wao halali na kuwataka mashabiki wa Klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi
kutokana na taarifa zinazodai kuwa amesaini kuichezea Yanga.
Vyombo
mbalimbali vya habari vya Tanzania hii leo vimeripoti OKWI ambaye ni raia wa Uganda
ameingia saini ya kuwachezea wapinzani wao wakubwa katika soka hapa nchini Yanga .
Makamu
Mwenyekiti wa Simba GEOFREY NYANGE KABURU amesema taarifa hizo si za kweli na
kwamba OKWI bado ni mchezaji wao halali na anamkabata utakaomalizika
June 30 mwakani.
Amesema
mshambuliaji huyo kwa sasa yupo Uganda akifuatilia Viza kwa ajili ya safari ya
kuelekea nchini Italia ambako anakwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa katika Klabu ya Parma inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama
Serie A.
Katika
hatua nyingine KABURU alimpigia simu OKWI na kuzungumza na Waandishi wa Habari moja
kwa moja kutoka Uganda ambaye nae alikanusha taarifa hizo huku wanahabari wakisikiliza mazungumzo hayo ambapo amedai kuwa akili yake kwasasa imejikita
zaidi kucheza soka la Ulaya na kama atashindwa majaribio yake atarejea Tanzania
na kuendelea kuitumikia Klabu yake ya Simba.
Katika hatua nyingine KABURU amevitaka vyombo vya habari vilivyo ripoti kuhusu Okwi kuhamia Yanga( gazeti la Bingwa na Spoti Starehe) kuomba radhi katika kipindi cha siku saba la sivyo uongozi wa utachukua hatua kali za kisheria dhidi yao.
"Tayari tumeshawasiliana na mwanasheria wa klabu ambaye ameelekeza kwamba ni lazima vyombo vya habari hivyo viombe radhi na viumbie umma kwamba vilisema uongo na vinajutia kosa hilo la kimaadili na habari hiyo itoke katika ukurasa wa mbele katika namna ileile ambayo habari ya leo ilitoka"
ROCKERSPORTS imemtafuta Katibu mkuu wa Yanga CELESTINE MWESIGWA kutaka kujua ukweli juu
ya kumsajili wa mshambuliaji huyo lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo
kwa kuwa kamati ya usajili ndiyo yenye mamlaka na masuala yote ya usajili.
No comments:
Post a Comment