KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 7, 2012

HAMISI 'DIEGO' KIIZA ATANGAZWA MWANAMICHEZO BORA WA MWEZI UGANDA.

Hamisi 'Diego' Kiiza akishangilia goli wakati wa michuano ya Kagame
Mshambuliaji wa mabingwa wa soka wa kombe la Kagame na timu ya taifa ya Uganda Hamisi “Diego” Kiiza ametangazwa kuwa mwanamichezo bora wa soka wa mwezi July nchini Uganda, tuzo ambayo hutolewa na chama cha waandishi wa habari za michezo humo(USPA).
Kiiza amepata mafanikio hayo kufuatia kuonyesha soka safi na la kuvutia katika michuano ya vilabu bingwa Afrika mashariki na kati(cecafa) ambayo si tu yaliisaidia timu yake ya Yanga kufanikiwa kutetea taji lao la michuano hiyo lakini pia alionekana kutakata kwa kuwa katika kiwango cha juu.
Hata hivyo wakati kwa upande wa Tanzania tuzo ya mfungaji bora ikiienda kwa Saidi Bahanuzi kufuatia kufunga jumla ya mabao sita, nchini Uganda kupitia chama hicho cha waandishi wa habari za michezo(USPA) wanasema Kiiza ndiye mfungaji bora wakisema amefunga jumla ya mabao 6 na alistahili kupata kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora(Golden boot).

 Mshambuliaji huyo wa zamani wa Nalubaale FC na URA FC katika tuzo hizo alipata alama 520 akimshinda kwa kwa mbali Julius Ogwang aliyepata alama 420 akimuacha kwa alama 100.
 Ogwang alikuwa katika kiwango cha juu katika mchezo wa kuwafuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana under-20 hasa katika mchezo dhidi ya Ghana “Black Satellites” mwezi uliopitaambapo alifunga mabao katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Nakivubo.
 Mchezaji bora aliyechukua nafasi ya tatu ni mcheza volley ball Lawrence Yakan ambaye aling’ara katika michezo ya kimataifa ya KAVC 2012. Lawrence alipata alama 415.
 

No comments:

Post a Comment