KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 7, 2012

Azam kutegua kitendawili cha mrithi wa Stewart John Hall leo.


Makamu mwenyekiti wa Azam Said Mohamed

Stewart John Hall liyetupiwa virago na Azam

Uongozi wa klabu ya Azam fc hii leo unatarajiwa kutegua kitendawili cha kocha wao mpya atakachukua mikoba ya mrithi wa Stuart John Hall aliyetimuliwa kazi baada ya kumalizika michuano ya kombe la Kagame.
Jumla ya makocha 12 kutoka sehemu mbalimbali nchini walituma maombi ya kutaka kazi hiyo ambayo Stewart Hall wiki iliyopita aliondolewa kutokana na kile kinachoonekana kwenda kinyume na maagizo ya waajiri wake.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Said Mohamed ametanabaisha kuwa wamepokea jumla ya maombi ya makocha 12 toka sehemu mbalimbali duniani lakini hii atatangazwa mmoja aliyeshinda vigezo ambavyo klabu hiyo inavihitaji.
  “tumepokea maombi kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanavyeti na uzoefu mkubwa katika kufundisha soka na kesho tutamtangaza”.
Mkataba wa Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi tarehe 31/07/2012.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame yakiwa ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia katika historia hiyo.
Stewart Hall ameacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atakaye tangazwa hii leo huku klabu hiyo ikisema mrithi wake atakayetangazwa atalazimika kufuata mfumo wa uchezaji ulioachwa na Stewart Hall kwani hiyo ndiyo Playing Philosophy ya Azam FC
Mrithi wa Stewart atakuwa anaungana na Kally Ongalla kama msaidizi wake ilhali Vivek Nagul  akirejea kufundisha timu ya 

No comments:

Post a Comment