Mabingwa wa
kombe la klabu Bingwa Afrika Mshariki na kati kombe la Kagame, timu ya Young
Africans Sports Club leo imepongezwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano
Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo.
Akiongea
katika Ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania mh,
Anna Makinda alisema anawapongeza wachezaji na viongozi wake wote, kwa
kuliletea Taifa ubingwa huo ambao timu 11 kutoka nchi wanachama zilishiriki.
Mh Makinda
alisema anafuraha siku ya leo kwa kuwa Bunge limetembelewa na wageni wengi,
wakiwemo watu mashuhuri na wageni maalumu timu ya Young Africans Sports Club.
Spika
alianza kwa kuwatambulisha Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Young Africans
wakiongozwa na mama mlezi wa klabu hiyo, Mama Karume, Francis Kifukwe kisha
akawatambulisha Mwenyekiti mpya wa Young Africans Yusuph Manji na makamu
mwenyekiti Clement Sanga.
Baada ya
hapo ilifuata zamu ya wachezaji na viongozi wakiwa na wazee wa klabu hyo,
makofi mengi mfululizo zaidi ya dakika moja yalipigwa kwenye meza baada ya
Nahodha Nadir Haroub Cannavaro kusimama na kuonyesha Kombe kwa watu wote na
wabunge waliokuwepo ndani ya bunge.
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya wabunge na mawaziri baada ya utambulisho wa
Young Africans ndani ya bunge, walitoka nje kwa pamoja na kupiga picha na
wachezaji na viongozi wa yanga wakiwa na kombe hilo la Kagame.
Baada ya
utambulisho, wabunge wanachama wa Young Africans waliwaalika wageni wao wote kupata kifungua kinywa katika
mgahawa wa bunge.
Wabunge
wanachama wa Young Africans waliandaa kikao cha mda mfupi ndani ya ukumbe wa
bunge la zamani (Msekwa Hall) ambapo wabunge, viongozi na wachezaji waliweza
kufahamiana kwa undani zaidi.
Mwenyekiti
Yusph Manji alifungua rasmi tawi jipya katika eneo la Bunge ambapo mwenyekiti
wa Yanga tawi la bungeni ni mh. Misanga, katibu mkuu wake akiwa ni Mh Godfrey
Zambi, mweka hazina mh.Martha Mlata huku Grace Kiwelu, Mwigulu Nchemba, Faki
Makame, Halima Mdee, na wengineo wakitajwa kama wajumbe katika uongozi huo.
Mh Captain
George Mkuchika ambaye jana aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamin wa
klabu, pia ndio aliyeteuliwa kuwa mlezi wa tawi la Young Africans bungeni.
Dua za
kubariki tawi hilo zilisomwa kwa pande zote mbili za dini kisha wabunge na
viongozi kupiga picha za pamoja, ambapo pia jioni ya leo wabunge wameaanda
futari kwa ajili ya wageni hao.
Timu
inatarajiwa kureje jijini Dar kesho kuendelea na maaandalizi ya msimu mpya wa
ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza septembe mosi.
No comments:
Post a Comment