|
Mwenyekiti wa Yanga Yusufu manji akiapishwa na mzee Jabir Katundu |
|
Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akiapa |
|
Haruni Nyanda mwanandinga wa zamani wa Yanga akiapa kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji |
|
George Manyama mjumbe wa kamati ya utendajia akiaapa |
|
Mama Fatma Karume akiwa na akina mama wa Yanga katika hafla ya kuapishwa na kusimikwa rasmi madarakani. |
|
Mlezi wa Yanga Mama Fatma karume katika picha |
|
Mama Fafma Karume |
|
Wanachama wa klabu ya Yanga wakifuatilia zoezi la kuapishwa viongozi wao |
|
Wajumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga katika picha ya pamoja na mama Karume na Fransis Kifukwe wajumbe wa baraza la wadhamini |
Kamati ya Utendaji na watendaji wengine wa Yanga katika picha ya pamoja
|
Manji akisalimiana na mama Fatma Karume |
|
Mama mlezi wa Yanga Fatma karume akiongea jambo katika hafla ya usimikaji viongozi wapya wa Yanga |
|
Mzee Jabir Katundu na mama Karume |
|
Fransis Kifukwe mjumbe wa baraza la wadhamini Yanga |
|
Mwenyekiti wa baraza la wazee la Yanga mzee Jabir Katundu |
|
Mama Fatma Karume na akina mama wa Yanga |
Kamati ya utendaji ya klabu
ya Yanga inayokutana katika makao makuu ya klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake
Yusufu Manji imemtangaza mheshimiwa George mkuchika kuwa mmoja wa wajumbe wa
baraza la wadhamni wa klabu hiyo.
Sambamba na mkuchika wengine waliochaguliwa ni Seif Ahmed na Ammi Mpungwe.
Isaack Chanji na Mohamed Nyengi wameteuliwa kuingia katika kamati ya utendaji huku jina moja likitafutwa kwa ajili ya kukamilisha idadi kamili ya wajumbe wa kamati ya utendaji.
Uamuzi huo umetolewa na
mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji katika mkutano wa kusimikwa rasmi madarakani
kwa uongozi mpya wa klabu hiyo zoezi ambalo linaendelea katika makao makuu ya
klabu hiyo chini ya mama mlezi wa Yanga mama Fatma
Karume.
Sambamba na hilo kamati
mpya ya utendeji ya klabu hiyo imeamua kufutilia mbali kamati zote ndogondogo
ndani ya klabu hiyo kuanzia leo isipokuwa kamati ya uchaguzi inayoongozwa na jaji John Mkwawa.
Katika kuhakikisha kunakuwepo na umoja zaidi katika maamuzi uongozi wa Yanga umesema utakuwa ukikutana na
viongozi wa matawi kila mwezi kwa lengo la kubadilisha
mawazo.
Katika mkutano wa kusimikwa kwa viongozi wapya wa klabu hiyo karibu viongozi wote wapya walikuwepo na kuapishwa na mwenyekiti wa baraza la wazee Ibrahim Katundu isipokuwa mjumbe Abdalah Bin Kleb ambaye alikuwa na hudhuru.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu manji amesema wanataraji kufanya sherehe ya kuchukua taji la Kagame baada ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani
No comments:
Post a Comment