George mkuchika mwenye suti. |
Kamati ya
utendaji ya klabu ya Yanga inayokutana katika makao makuu ya klabu hiyo chini
ya mwenyekiti wake Yusufu Manji imemtangaza mheshimiwa George mkuchika kuwa mmoja
wa wajumbe wa baraza la wadhamni wa klabu hiyo.
Uamuzi huo
umetolewa na mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji katika mkutano wa kusimikwa rasmi
madarakani kwa uongozi mpya wa klabu hiyo zoezi ambalo linaendelea katika makao
makuu ya klabu hiyo chini ya mama mlezi wa Yanga mama Fatma Karume.
Sambamba na
hilo kamati mpya ya utendeji ya klabu hiyo imeamua kufutilia mbali kamati zote
ndogondogo ndani ya klabu hiyo kuanzia leo.
Katika
kuhakikisha kuna kuwa na umoja zaidi katika maamuzi uongozi wa Yanga umesema
utakuwa ukikutana na viongozi wa matawi kila mwezi kwa lengo la kubadilisha
mawazo.
Taarifa
zaidi itafuata……………….
No comments:
Post a Comment