|
Makamu mwenyekiti wa Simba Nyange Kaburu. |
Mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba ya jijini Dar
es Salaam wanataraji kuumana dhidi ya City Stars ya Kenya katika mchezo wa
kusheherekea siku ya Simba maarufu kama Simba day mchezo ambao utapigwa katika
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Kila mwaka ifikapo tarehe 8 mwezi wa 8 klabu hiyo
imejenga utamaduni wa kufanya sherehe maalum ambayo wanachama na wapenzi wa
klabu hiyo hujumuika kwa pamoja kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja
na wachezaji wa timu hiyo kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kuwatembelea
wagonjwa mahospitalini na kugawa misaada ya vitu mbalimbali.
Mbali na hayo sherehe hiyo ukamilishwa na burudani ya
soka ambapo klabu hiyo inatumia fursa hiyo kuwatambulisha wachezaji wao na
jezi mpya kwa ajili ya msimu mpya wa kimashindano.
Akiongea na Rockersports makamu mwenyekiti wa klabu
hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema safari hii wameamua kuialika timu ya City
Stars toka nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa kusheherekea siku hiyo muhimu.
Akitoa sababu ya kuialika City Stars Kaburu amesema wameshindwa kupata timu nyingine zaidi hiyo kufuatia nyingi kuwa katika ligi za nchi zao na hivyo imekuwa vigumu kupata nafasi ya kuja nchini kwa ajili ya mchezo huo.
Upande wa kutembelea wagonjwa amesema watatembelea hospitali na mwananyala na Amana za jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment