Manchester United
yamjumuisha Vidic ziara ya ulaya
Nemanja Vidic amejumuishwa katika
kikosi cha wachezaji 21 cha Manchester United kwa ajili ya michezo ya
matayarisho ya kuanza kwamsimu barani ulaya.
mlinzi huyo raia wa Serbia na ambaye
ni tegemeo kubwa Old Trafford alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisumbuliwa
na majeraha aliyo yapata katikati ya msimu uliopita.
Washindi hao wa pili wa ligi kuu ya
nchini Uingreza wanataraji kucheza dhidi ya Valerenga hapo kesho na baadaye
kuelekea Gothenburg kucheza dhidi ya Barcelona
August 8 kabla ya kumaliza dhidi ya Hannover 96 August 11.
Majina ya nyota waliojumuishwa katika
hicho cha mashetani wekundu ni pamoja na Wayne Rooney, Ashley Young na Rio
Ferdinand.
Jumla ya wachezaji 21 wamekifanya
kikosi cha sasa kuwa kizuri zaidi kuliko kikosi kile kilicho fanya ziara ya
nchini Afrika kusini mwezi July.
Wengine ni wachezaji walioko katika
kikosi cha GB ambao ni Ryan Giggs ,Tom Cleverley na mlinzi mbrazil Rafael kwa
kuwa wako katika kikosi GB kinashiriki michezo ya Olympic jijini London.
Official: Aquilani
ajiunga na Fiorentina akitokea Liverpool
Kiungo wa Liverpool Alberto Aquilani
amejiunga na Fiorentina ya Italia hizi zikiwa ni taarifa zilizo thibitishwa na
pande zote mbili.
Baada ya kujiunga na Merseyside mwaka
2009, Aquilani ambaye alinunuliwa kwa kwa ada ya uhamisho ya pauni mlioni 17
ameichezea timu hiyo michezo 18 tu katika ligi
Mipango ya kuuzwa kwake ilikuwa wazi
kufuatia kuondoshwa katika kikosi ambacho kimekuwa katika ziara ya maandalizi
ya kuanza kwa ligi huko Amerika ya kaskazini.
Liverpool imethibitisha hilo kupitia
mtandao wa klabu hiyo ilhali Rais wa Fiorentina Andrea Della Valle akiwaambia
wanahabari huko Moena iliko kambi ya Fiorentina akisema kuwa wamefanikiwa
kumchukua Aquilani.
Hapo kabla ya ilidhaniwa kuwa chini
ya utawala mpya wa Brendan Rodgers huenda mtaliano huyo angepewa nafasi kubwa
kikosini hasa baada ya kutumikia misimu miwili ya mwisho kwa mkopo katika
vilabu vya AC Milan na Juventus.
Bosi wa zamani wa Swansea tayari
ameweka wazi kuwa klabu yake hiyo inafikiria kupata saini za Loe Allen wa
Swansea na Clint Dempsey wa Fulham lakini huenda Andy Carroll akaondoka Anfield.
Penati ni
bahati anasema Ronaldo
Mfumania nyavu huyo alipoteza penati yake akiwa ni
mpigaji wa kwanza katika mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya Real Madrid
wakicheza dhidi ya Bayern Munich na katika mchezo wa mataifa ya Ulaya Euro 2012
Hispania dhidi ya Ureno hakupata nafasi ya kupiga kwa kuwa alichagua penati ya
mwisho.
amenukuliwa akisema
"kwangu penati huwa sina bahati nazo, kwa hiyo
naweza kusema nimekuwa sina bahati katika sehemu hiyo fupi lakini muhimu
kimatokeo.
"mtu anaweza mawazo yake kama kupiga ya kwanza
,ya pili au ya mwisho lakini mwisho wa siku inakuwa ni bahati na sibu".
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 27
amefunga jumla ya mabao 46 katika ligi kuu ya soka nchini Hispani maarufu La Liga
katika jumla ya michezo 38 msimu wa 2011-12.
No comments:
Post a Comment