Afisa habari wa Yanga Luis Sendeu katikati akitoa utambulisho wa Didier Kavumbangu kushoto ni Said Bahanuzi |
Kavumbangu akitoa neno lake la moyoni kwa mashabiki waliomlaki hii leo nje ya makao makuu ya klabu ya Yanga. |
Saidi Bahanuzi akiongea na mashabiki wa timu ya Yanga makao makuu ya klabu hiyo Jangwani. |
Utambulisho
wa Kavumbagu umefanywa na afisa habari wa Yanga Luis Sendeu ambaye amesema
mchezaji huyo ameingia mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo yenye
maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na amekabidhiwa jezi
nambari 21.
Akiongea na
wanahabari Kavumbagu mwenyewe amesema kuwa amefurahia kujiunga na klabu hiyo
ambayo ni kubwa Afrika mashariki na kwamba atatumia uwezo wake wote kuitumikia
na kuipa mafanikio.
Pia
amefurahishwa na namna alivyopokewa na mashabiki wa klabu ambao wameonyesha kuwa
na imani naye na yeye akiahidi kuwa hatawaangusha.
Kavumbangu aliwasili rasmi nchini usiku wa jana na hii leo ameanza mazoezi na timu ya Yanga yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Loyola iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam.
Kavumbangu aliwasili rasmi nchini usiku wa jana na hii leo ameanza mazoezi na timu ya Yanga yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Loyola iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam.
Aidha msemaji
wa Yanga Luis Sendeu amesema klabu ya Yanga kesho saa nne asubuhi itawasimika
madarakani rasmi viongozi wapya wa klabu hiyo na usimikaji huo utaongozwa na mama Fatma
Karume ambaye ni miongoni mwa wadhanini wa klabu hiyo, hafla ambayo itafanyika
makao makuu ya klabu hiyo.
Hafla hiyo
itafuatiwa na kikao cha kwanza cha kamati ya utendaji tangu viongozi hao
kuingia madarakani wakiongozwa na mwenyekiti wao Yusufu Manji na baadaye saa nane
mchana kabla ya timu ya Yanga itaanza safari ya kuelekea Bungeni kulipeleka kombe la
Kagame ikiwa ni ombi la baadhi ya wabunge ambao ni wapenzi wa klabu hiyo.
Wakati hayo
yakiwa hivyo mshambiliaji wa mabingwa hao wa kombe la Kagame Said Bahanuzi ametumika
mkutano huo wa utambulisho wa Kavumbagu kukanusha taarifa zilizo zagaa kuwa amejiunga
na mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba.
Bahanuzi
amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba yeye ni mchezaji wa Yanga
na ana mkataba wa miaka miwili na atautumikia mpaka umalizike.
Katika hatua
nyingine viongozi wa klabu hiyo wanatarajiwa kumzawadia mfungaji bora wa
michuano ya kombe la Kagame Said Bahanuzi ambaye alimaliza michuano hiyo
akifunga jumla ya mabao 6.
No comments:
Post a Comment