Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam Mrisho Ngassa
ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari katika klabu yake mpya ya
Simba ambayo imeingia naye mkataba wa mwaka mmoja.
Ngassa ambaye katika siku za karibuni amekuwa gumzo
miongoni mwa wapenzi wa soka kutokana na vitendo alivyovionyesha katika
michuano ya Kombe la Kagame na kupelekea Azam kuamua kumuuza.
Awali ilitarajiwa mchezaji huyo angeuzwa kwenda
klabu ambayo inasemekana ana mapenzi nao ya Yanga lakini katika hali ya
kushangaza Azam iliamua kumpeleka Simba kitendo mwenyewe alidai hakuridhishwa
nacho.
Akizungumza na waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti
wa Simba, Godfrey Nyange-Kaburu amesema kuwa uhamisho wa mchezo huyo umetokana
na maelewano ya pande zote tatu yaani Azam, Simba na Ngassa mwenyewe yaliyofikiwa.
Kaburu amesema kuwa mchezaji huyo amekabidhiwa jezi
namba 16 na anatarajiwa kuonekana katika michezo mbalimbali ya timu hiyo
ikiwemo ya kirafiki na Ligi Kuu ambayo inatarajiwa kuanza baadae mwezi huu.
Hatua hiyo ya kusajiliwa Ngasa imekuja imetimiza za
kocha wa Simba Milovan ambaye alikuwa ana tamani kuwa na Ngasa katika kikosi
chake.
Kaburu aliwaomba washabiki wa Simba kumpokea
mchezaji huyo kwa mikono miwili kwani amekwenda hapo ili kufanya kazi na
kuiletea klabu hiyo vikombe zaidi hivyo wawe na imani nae.
Ngassa mwenyewe akihojiwa amesema kuwa ameenda
katika klabu hiyo kufanya kazi na kuahidi kuifanyia makubwa klabu hiyo na kuwaomba
viongozi na mashabiki wa klabu hiyo kumpa ushirikiano ili aweze kufikia nia
yake.
Wakati huohuo badhi ya mashabiki wachache
waliohojiwa kuhusiana na suala hilo wameonyesha kutokuwa na imani na Ngassa
kama ataitumikia klabu hiyo kwa moyo kutokana na kuonyesha mapenzi ya wazi kwa
Yanga ambao ni mahasimu wao wakubwa.
Mashabiki wamesema kuwa toka mchezaji huyo amehama
Yanga kwenda Azam hatajawahi kuifunga timu ya Yanga katika michezo ambayo
wamekutana hivyo kuwa na mashaka kama anaweza kufanya hivyo akiwa na Simba.
Kaburu amedai klabu hiyo imenunua mkataba wote
aliokuwa nao Azam ambao ni wa mwaka mmoja kwa makubaliano maalumu ambayo
hakutaka kuyaweka wazi.
No comments:
Post a Comment