Mabao mawili
yaliyofungwa na mshambuliaji Khamis Mcha Khamis yalitosha kuipa ushindi timu ya
taifa ya Zanzibar dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda( Amavubi) katika mchezo wa
kundi C uliopigwa uwanja wa Namboole jioni
ya leo.
Mshambuliaji
huyo alitumia makosa ya mlinda mlango wa Rwanda Jean Claude Ndori kushindwa
kuondosha mpira wa pasi ya kurejeshwa kwa mlinda mlango huyo kunako dakika ya 8
ya mchezo.
Tangu wakati
huo Zanzibari ilitawala mchezo na
pengine ingeongeza bao lingine katika kipindi cha kwanza lakini umaliziaji
mbaya pengine kutokana na uwanja kuwa na matope.
Katika kipindi
cha pili Amavubi ilirudi na ari nyingine kwa lengo la kusawazisha bao kupitia
kwa Jean Baptiste Mugiraneza na Haruna Niyonzimana lakini mlinda mlango wa Zanzibar
Mwadini Ally alikuwa imara kuzuia mipira ya hatari.
Zanzibar iliandika
bao la pili kupitia tena kwa Khamis Mcha Khamis baada ya kupokea mpira wa
shambulizi la kushtukiza kunako dakika ya 62 akipokea pasi ya nzuri kutoka kwa Kassim
Suleyman toka upande wa kulia wa uwanja.
Rwanda haikukata
tama na juhudi zao zilizaa matunda zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kumalizika
kwa bao Dady Boril aliyetokea benchi.
Mchezo huo uliwakutanisha manahodha wawili wa timu hizo za taifa ambao wote wanachezea timu moja ya Yanga ambao kabla ya mchezo kuanza walisalimiana kabla ya kubadilishana bendera za mataifa yao.
Katika mchezo
mwingine wa kundi hilo la C Malawi iliichapa Eritrea mabao 3-2 na hivyo kufanya
kundi hilo kuwa katika mlingano unaofanana kwa maana ya timu ina nafasi ya
kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
Zanzibar
inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 4 ambapo Rwanda na Malawi zikifuatia huku
kila moja ikiwa na alama 3 na Eritrea ikiwa na alama 1.
No comments:
Post a Comment