Timu za
taifa za Tanzania Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heoroes zimefanikiwa kutinga
nufu fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Challenge Cup 2012 na sasa zitakutana
wenyewe kwa wenyewe kusaka timu itakayo cheza fainali ya michuano.
Kilimanjaro
yenyewe imeichapa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi ‘ kwa mabao 2-0 katika
mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Lugogo.
Kilimanjaro ilipata
mabao yake kupitia kwa kwa Amiir Kiemba na John Raphael Bocco mabao
yaliyopatikana kipindi vipindi viwili tofauti.
Mchezo ulianza
taratibu kwa timu zote mbili, kabla ya Amiir Kiemba kuandika bao la kwanza
kunako dakika ya 34 ya mchezo.
Alifunga bao
hilo baada ya kupata pasi ya krosi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto kutoka upande wa
kushoto wa uwanja baada ya kumtoka mlinzi wa Rwanda.
Kilimanjaro
ilitawala mchezo na pengine wangeongeza bao lingine baada ya Mrisho Ngassa kushindwa
kuunganisha krosi ya Kevin Yodan kutoka upande wa kushoto.
Baada ya
mapumziko John Raphael Bocco aliandika bao la pili kunako dakika ya 54 baada ya
kuunganisha mpira ulio temwa na mlinda mlango wa Rwanda Jean Claude Ndori.
Ndori alitema
mpira uliopigwa umbali wa mita 35 na Mwinyi Kazimoto na hivyo kuandika bao lake
la 5 katika michuano hii.
Licha ya
Rwanda kufanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Kilimanjaro katika dakika za
mwisho, lakini bado ulinzi wa Kevin Yodan na Shomari Kapombe ulisaidia kuzuia
Rwanda kuandika hata bao moja.
Kwa matokeo
hayo ni kwamba Kilimanjaro Stars itakutana na ndugu zao wa Zanzibar Heroes, mabingwa
wa mwaka 1995 ambao katika mchezo wa robo fainali ya pili wamefanikiwa
kuwafunga Burundi (Intamba Murugamba) kwa penati 6-5 baada ya dakika 90 za
mchezo huo kumalizika bila kufungana.
Abdallah
Othman alifunga penati ya ushindi kwa Zanzibar baada ya Fiston Abdoul wa
Burundi kupoteza penati yake
Nahodha wa Burundi
Selemani Ndikumana na nahodha Zanzibar Nadir
‘Cannavaro’ Haroub walokosa penati zao.
Ndani ya
dakika 90 mshambuliaji wa Zanzibar Juma Jaku Juma alipoteza nafasi nyingi za
kumalizia huku mlinda mlango Ally Mwadini akiokoa mipira mingi iliyo elekezwa
langoni kwake na Selemani Ndikumana na Christopher Nduwagira.
Penati za
Zanzibar zilifungwa na Khamis Mcha Khamis, Adeyom Saleh Ahmed, Juma Jaku Juma,
Nuhu Haji Samih, Aggrey Morris na Abdallah Othman wakati ambapo kwa upande wa
Burundi penati zao zilifungwa na Styve Nzigamasabo, Amisi Tabwe, Christopher
Nduwagira, Leopold Nkurikiye na Gael Duhatindayishimiye.
No comments:
Post a Comment