Shirikisho la
soka duniani fifa wiki ijayo linatarajiwa kutoa majibu ya mgogoro wa uchaguzi
wa chama cha soka nchini Tanzania TFF ambapo pia litaweka wazi majibu ya nani
atasimama katika uchaguzi huo.
Ujumbe maalumu wa fifa umekamilisha kazi yake ya uchunguzi juu ya sakata hilo hilo hii
leo.
Ujumbe huo ulikuwa nchini chini kwa siku mbili chini ya Primo Covarro, ambapo walikuwa
wakichunguza hali ya mambo juu ya sakaa hilo ambapo liipitia mchakato mzima wa
uchaguzi na kukamilisha kazi hiyo hii leo.
Akiongea na
waandishi wa habari Covarro amesema "Nimekutana na kusikiliza wagombea
wote walioenguliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF, maafisa wa serikali na wengine
wote walihusika katika mchakato huo wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa shirikisho
la soka nchini TFF".
"Sisi
sio watoaji wa maamuzi, kazi yetu ni kuwasilisha ripoti Fifa na Caf, na maamuzi
yatatolewa na ndani ya kipindi cha wiki moja"
Mgogoro wa
uchaguzi uliibuka wakati kamati ya uchaguzi ilipowaengua wagombea kadhaa
akiwemo aliyekuwa katibu wa zamani wa Yanga Jamal Malinzi.
Malinzi
alikosa sifa kutokana na kukosa sifa ya kuongoza shughuli za soka ndani ya
kipindi cha miaka mitano mufululizo hali iliyo sababisha nafasi ya mgombea wa nafasi ya Rais
kusaliwa mgombea mmoja Athuman Nyamlani ambaye amekosa mpinzani.
Naye katibu wa
zamani wa TFF Michael Wambura, ambaye alikuwa akiwania nafasi ya makamu wa Rais
pia aliondolewa na kamati ya rufaa ya uchaguzi kutoka na kukosa
uadilifu jambo ambalo alilipinga vikali.
Uchaguzi huo
ulisimamishwa FIFA mwishoni mwa mwaka jana ambapo Rais wa sasa wa TFF President
Leodegar Tenga anaendelea kuongoza mpaka hapo uchaguzi huo utakapo kamilika.
No comments:
Post a Comment