Licha ya kustaafu lakini bado mashabiki wake wanampenda kiasi kufurika katika jiji la Shangai na kupelekea watu watano kujeruhiwa akiwemo afisa wa polisi.
Katika ratiba yake ya hii leo Beckham alikuwa atembelee chuo kikuu cha Shanghai cha Tongji.
Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid alikuwa akutane na wachezaji wa timu ya chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba kuitangaza ligi kuu ya China inayotambulika kama Chinese Super League.
Hata hivyo kufuatia umati mkubwa kujitokeza kwa lengo la kumlaki kiungo huyo wa zamani wa England kumepelekea zoezi hilo kushindikana ambapo baadaye aliomba radhi mashabiki wake hao kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na Sina Weibo.
Kabla ya vurugu kujitokeza: Maelfu wajitokeza wakati David Beckham alipowasili chuo kikuu cha Shanghai.
Afisa usalama akilazwa chini kwa huduma ya kwanza.
Maafisa usalama walishindwa kuzuia vurugu hizo ambapo walikuwa wakisonga mbele licha ya kuwekewa kizuizi.
Katika ujumbe wake Beckham amenukuliwa akisema
'Samahani sikuweza kutokea uwanjani kuiona timu ilikuwa ni vigumu kupenya katikati ya mashabiki. Nimesikia kulikuwepo na watu waliojeruhiwa, Nina matumaini wako salama nawataki wapone haraka'
Takribani watu 1,000 inaaminika walikuwa wakitaka kumkaribia Beckham na polisi wamethibtisha kuwa maafisa wake watatu walijeruhiwa katika vurugu hizo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 38 alistaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuisaidia Paris-Saint Germain kutwaa taji la ligi ya Ufaranza maarufu kama Ligue 1.
No comments:
Post a Comment