KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, June 29, 2013

KUELEKEA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA MABARA UWANJA WA MARAKANA HAPO KESHO UKWELI NDIO HUU.


Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema kikosi chake hakina majeruhi hata mmoja baada ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uruguay na huenda akatangaza kikosi kilekile kilichocheza katika mchezo wa nusu fainali kuanza katika fainali ya hapo kesho.
Hulk mpaka sasa ameshindwa kuweka mpira wavuni katika jumla ya michezo tisa ya kimataifa hii ikiwa ina maana kuwa nafasi yake kuaza kikosini ni finyu ikilinganishwa na wakali kama Bernard na Lucas Moura.
Roberto Soldado na Cesc Fabregas katika kikosi cha Hispania walikosekana katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Italia kutokana na maumivu madogo ya msuli hivyo inanyoonekana ni kwamba wachezaji hao wawili wanaweza kuanza hapo kesho.

MATCH PREVIEW
Hispania wametajwa kama ni timu ambayo imetinga hatua hiyo kwa bahati sana lakini wengine wanasema ni fainali iliyokuwa katika ndoto za wapenzi wengi wa soka ni itakuwa na mvuto wa aina yake pale Maracana .
Wakati Italia ikitajwa kuwa ndiye aliye onyesha upinzani wa kweli kwa Selecao ukweli ni kwamba  Azzurri walisha kutana mara mbili na Brazil mwaka huu lakini bado mawaidha ya wengi ni kwamba hii itakuwa ni "dream final" baina ya Brazil na Hispania.
Brazil na Hispania kwa ajabu ya wengi kwamba wamekutana mara moja tu katika kipindi miaka 23 iliyopita na hiyo ilikuwa ni mwaka 1999 katikia mchezo wa kirafiki ambao walikwenda sare ya bila kufungana.
Tangu wakati huo Hispania imekuwa ikifanya vizuri na kuwachapa yeyeto anayetokeza.
Brazil ndiyo taifa ambalo ni kubwa kisoka anayedaiwa kulinganishwa naye kama mbabe na mchezo huu unatazamwa kama ndiyo kipimo tosha kwa mataifa hayo.
Ushindi wa Hispania dhidi ya Brazil ambao hawajapoteza katika uwanja wa nyumbani tangu mwaka 1975, utadhihirisha ukubwa wao katika soka la dunia ya leo.
Vuta kumbukumbu miaka 63 iliyopita ambapo Hispania ilibamizwa kwa kichapo cha karaha cha mabao 6-1 katika dimba la Maracana matokeo ambao yaliondoa matumaini yao ya kutwaa kombe la dunia mwaka 1950 na kusalia katika kumbukumbu kuwa ni kichapo kikubwa mno kuwahi kuwakumba katika michuano mikubwa.
Kwa kuongezea hili la faida ya kucheza katika uwanja wa nyumbani Brazil itafaidika na hilo.
Kocha wa Hispania Vicente del Bosque anasema mchezo mgumu dhidi ya Italia wa nusu fainali umeivuruga kambi yake lakini wanasonga mbele.

Brazil's record against Spain
  • 1934 World Cup first round: Lost 3-1
  • 1950 World Cup final round: Won 6-1
  • 1962 World Cup group stage: Won 2-1
  • 1978 World Cup: Drew 0-0
  • Friendly, 1981: Won 1-0
  • 1986 World Cup: Won 1-0
  • Friendly, 1990: Lost 3-0
  • Friendly, 1999: Drew 0-0

No comments:

Post a Comment