Kiungo wa AC Milan Ricaldo Kaka ameitaka klabu yake hiyo isimlipe chochote wakati huu ambapo anahaha kuponya majeraha ya msuli aliyo yapata katika mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na kikosi hicho.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Barazil mwenye umri wa miaka 31, alilazimika kubadilishwa katika dakiki ya 70 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Torino.
Kaka alijea kikosini msimu huu baada ya kuihama klabu yake na kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa rekodi ya dunia £56 mwaka 2009.
Amenukuliwa akisema
"Sitaki chochote kutoka Milan, isipokuwa upendo na kuungwa mkono mpaka nitakarejea kuwa fiti na kuwa tayari kwa kucheza"
"Kwa maana hiyo nimeamua kusimamisha malipo yangu kipindi hiki. Ninachokitaka ni kuungwa mkono na kusaidiwa kupona sawasawa.
"Ni kipindi kigumu lakini nimeanza kurejea vizuri na nina matumaini nitarejea haraka "
Kaka ameongeza kwa kusema kuwa ameongea na Rais wa Milan
Adriano Galliani na madaktari wa timu kwa kirefu kabla ya kuamua kuacha kulipwa.
Bado haijawekwa wazi kama Milan wamekubaliana na maombi hayo ya Kaka.
Kaka alikuwa ni mchezaji bora wa dunia mwaka 2007 na aliitumikia klabu hiyo kwa michezo 268
kati ya mwaka 2003 na 2009, na kufunga jumla ya magoli 95.
Aliisaidia kushinda taji la Serie A mwaka 2004 na 2007 walitwaa klabu bingwa ulaya.
No comments:
Post a Comment