Bosi wa Tottenham Tim Sherwood amekanusha taarifa kuwa amekuwa katika mazungumzo ya kumnunua kwa mkopo mlinzi wa Manchester City Joleon Lescott.
Mlinzi huyo wa kati ambaye amekuwa si pendekezo katika kikosi cha kwanza ndani ya Etihad
Stadium, amekuwa akihusishwa na safari ya kuelekea London ya Kaskazini mpaka mwisho wa msimu.
Hata hivyo Sherwood amesema hana mpango wa kuongeza nguvu kikosi chake katika dirisha hili la usajili la mwezi wa Januari, akisisitiza kuwa atakazania zaidi katika kukiimarisha kikosi chake katika ubora wa uchezaji na 'fittness'.
‘Sidhani kama tunahitaji mchezaji hapa. Tunahitaji uimara zaidi wa kikosi kwa wachezaji tulionao'.
No comments:
Post a Comment