Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameng'aka juu ya tetesi kuwa klabu yake imekuwa katika mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain.
Mreno huyo ameripotiwa kuwa anafikiria kufanya usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Argentina mwezi Januari ambaye ameshatupia nyavuni jumla yan mabao 13 kwa klabu yake ya sasa msimu huu na huku akikumbukwa kwa mabao 48 aliyoweka wavuni akiwa chini ya Mourinho wakati huo wakiwa pamoja katika klabu ya Real Madrid.

Hata hivyo meneja wa Chelsea ametupilia mbali madai hayo na kusisitiza kuwa hajawahi hata kidogo kuwasiliana na Napoli juu ya mpango huo.
Alipoulizwa kama kuna mpango kama huo kuhusu Higuain, Mourinho aling'aka kwa wanahabari "No no no."
No comments:
Post a Comment