KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 14, 2013

Manchester United yavunja rekodi yake ya mapato ndani ya kipindi cha robo ya mwaka.

  Manchester United imeweka rekodi ya ongezeko la mapato yake kwa asilimia 29.1 na kufikisha kiasi cha pauni milioni £98.5 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka.

Kufuatia kupata udhamini mpya wa makampuni 12 kutoka Ulaya na kote duniani ikiwa ni pamoja na udhamini wa shirika la ndege la Urusi la Aeroflot na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi, mapato yatokanayo na biashara imepanda na kukusanya kiasi cha pauni milioni £16.9 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya mwaka uliopita.

Makusanyo yatokanayo na haki ya matangazo pia yameonekana kuongezeaka na kufikia pauni milioni £5.6 ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka uliopita kupitia michezo ya ligi kuu 'Premier League' na Vilabu bingwa Ulaya.

Makamu mwenyekiti wa United Edward Woodward amenukuliwa akisema
“Tunayo furaha kufikia mafanikio ya rekodi ya mapato kwa robo ya kwanza ya mwaka, hiyo imetokana na utanuzi wa biashara mapato ya haki za matangazo ya vyombo vya habari.

“aina hii ya kipee ya makabiliano ya kibiashara itaendelea ili kukua zaidi hapo baadaye.”

United pia inaweza kufaidika kutoka kampuni ya BT kiasi cha pauni £897 endapo itapata dili la haki ya matangazo ya michezo yake ya ligi ya mabingwa Ulaya na Europa League kwa kipindi cha miaka miatatu kuanzia mwaka 2015.
Woodward anasema
“pia tunapata faraja na furaha kubwa kwa kuendelea thamani kimichezo kufuatia tangazo la hivi karibuni la BT kupata haki ya UK kutangaza moja kwa moja michezo yetu ya Champions League na Europa League kwa miaka mitatu kuanzia msimu wa 2015/16”.

No comments:

Post a Comment