Nahodha wa Bayern Munich Philip Lahm amesema kikosi chake kinampango wa kuvunja rekodi ya Barcelona ya kuwa mabingwa mara nyingi wa Champions League wakati ambapo wanajipanga kwa mchezo wa leo dhidi ya CSKA Moscow hii leo.
Die Roten wanaelekea katika mchezo huo wakiwa wameshinda michezo nane ambayo ambayo ni kama ilivyo kwa Barca.
Die Roten wanaelekea katika mchezo huo wakiwa wameshinda michezo nane ambayo ambayo ni kama ilivyo kwa Barca.
Lahm anasema licha ya mabingwa watetezi kuwa tayari wamefuzu kwa hatua ya mtoano, kinacho wapa nguvu ni kuweka historia na wamejipanga kufanya vema mjini Moscow.
Amenukuliwa Lahm akisema
"huu ni mchezo muhimu kwetu tunataka kuweka rekodi na kusonga mbele zaidi kama itawezekana."
Kocha wa Bavarians Pep Guardiola amesisitiza kuwa utakuwa ni mchezo mgumu kwa upande wake hususani baada ya nguvu kubwa kutumika kumchapa mpinzani wake mkubwa Borussia Dortmund bao 3-0 mwishoni mwa wiki.
Winga wa Bayern Arjen Robben mwenye umri wa miaka 29 ameongeza kwa kusema

"Tunajiamini kwa kiasi kikubwa baada ya mchezo dhidi ya Dortmund lakini tunajua mchezo huu utakuwa mgumu"
No comments:
Post a Comment