KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 27, 2013

Kolo Toure anasema Sergio Busquet wa Barca si lolote kwa ndugu yake Yaya dimba la kati.

Mlinzi wa Liverpool Kolo Toure anaamini kuwa Barcelona walifanya makosa ya kumuuza kaka yake Yaya Toure ambaye anaamini kuwa ni bora zai ya Sergio Busquets.

Kolo ambaye alijiunga Anfield majira ya kiangazi baada ya kukosa nafasi katika klabu yake ya zamani ya Manchester City anaona kuwa kwa kuwalinganisha ndugu yake ni bora zaidi.
Yaya aliondoka Camp Nou na kujiunga na Blues msimu wa 2010.

Amenukuliwa akisema kuwa 
"nimekuwa na uzoeufu kama wa Yaya," 
"Makocha hujiunga na klabu na kuleta wachezaji wale wanaowataka kwa gharama yoyote hata kama ni mzuri ama si hivyo.

"Yaya alikuwa mzuri zaidi ya Sergio Busquets ndani ya Barcelona lakini alikuwa nyuma yake na ilikuwa ngumu kwake kukubali.

"Nilimshauri kujiunga na Manchester City nilipokuwa bado nipo pale. Alinisikiliza kaka yake mkubwa na sasa ni bosi mkubwa katika dimba la kati."

Kolo amecheza michezo nane tangu kuanza kwa msimu huu akiwa katika klabu yake mpya na ambayo ipo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya England na Kolo anaamini amedhihirisha kitu kwa City.

No comments:

Post a Comment