KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 22, 2013

Southampton watuma salamu kwa Arsenal

Southampton ambao wameonyesha ukali watakumbana na kibarua chao kigumu zaidi katika Ligi ya Premia msimu huu Jumamosi watakapokutana na Arsenal ugenini.
Hata hivyo, hilo halimbabaishi hata kidogo meneja Mauricio Pochettino, na wala haliwatishi mastraika wake matata Rickie Lambert na Jay Rodriguez.
Saints au Watakatifu ukipenda wamo nambari tatu kwenye ligi baada ya kucheza mechi 11, wakiwa na alama 22 ambazo ni tatu tu chini ya zile walizo nazo Arsenal ambao wanaongoza ligi.
Lakini Pochettino anaamini kwamba Saints wanaweza kuwalima viongozi hao wa ligi sawa na walivyowafanyia Liverpool walipokuwa wakiongoza ligi mapema kwenye msimu.
"Ninafikiri itakuwa mechi sawa na ya Liverpool kwa sababu tulipokuwa tukicheza nao walikuwa juu kwenye ligi,” raia huyo wa Argentina aliambia televisheni ya Southampton ya Saints Player mnamo Alhamisi.
“Daima tumeamini kuwa tunaweza kushinda kila mechi tunayocheza. Tunaamini kwamba tunaweza kucheza vyema sana kwenye mechi na tunaweza kupata matokeo mazuri kutoka kwenye mechi hii – daima sisi huamini hivyo,” akaongeza, akisisitiza imani ambayo imeiinua klabu hiyo kutoka pwani ya kusini katika kiwango cha kadiri kwenye ligi kuu.
Pambano hilo linakuja baada ya muda wa mapumziko kwa ajili ya mechi za kimataifa ambapo wachezaji watatu wa Saints waliitwa kuchezea Uingereza kwenye mechi dhidi ya Chile na Ujerumani - Lambert, Rodriguez na nahodha Adam Lallana.
Pochettino alisema Waingereza hao watatu wako vizuri kufanya vema ndani ya klabu. “Nina furaha sana kutokana na uchezaji wao walipokuwa wakichezea timu ya taifa,” alisema licha ya Uingereza kuchapwa mechi zote mbili.
“Nina uhakika kwamba uzoefu huo utawafaa sana kwa sasa na siku zijazo katika timu na pia labda katika timu ya taifa.
“Ni bayana kwamba msukumo na uzoefu waliopata wakichezea timu ya taifa vitatusaidia hapa Southampton pia."
Lambert, aliyengoza safu ya mashambulizi Saints waliposhindwa 6-1 uwanjani Emirates msimu uliopita, alisema anasubiri kwa hamu na ghamu kurekebisha mambo.
“Nasubiri sana Jumamosi kwa sababu tunafanya vyema kwa sasa na ni matumaini yetu kwamba tunaweza kupeleka uzuri huu kwenye mechi hiyo,” 
 Aliambia tovuti ya Southampton.
"Tutaenda huko tukiwa na imani. Tunajua itakuwa moja ya mechi ngumu zaidi kwa sababu Arsenal wanacheza vyema kwa sasa.
 Itakuwa ngumu, lakini tuna imani kwamba tunaweza kwenda huko na kutoka na kitu.”
Rodriguez alieleza imani yake kwamba timu hiyo itafanya vyema msimu uliopita.
“Tutapelekea Arsenal mchezo na itakuwa mechi ngumu,” alisema. “Mwaka uliopita ulikuwa jinamizi kwani tulichapwa 6-1 huko, lakini tuna ujumbe tunataka kufikisha na tutafika huko tukikusudia hilo.”

No comments:

Post a Comment