Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo asubuhi katika fukwe za Coco |
Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara Young
Africans leo wameendelea na mazoezi kwa kujifua katika fukwe za Coco
kujiandaa na mchezo wa Hisani "Nani Mtani Jembe" dhidi ya Simba SC
Disemba 21, 2013 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha mholanzi Ernie Brandts baada ya kufanya mazoezi ya
uwanjani kwa kipindi cha takribani wiki mbili, leo kilikuwa kikijifua
katika fukwe za Coco ambapo mazoezi ya stamina, na viungo ndio yalitwala
zaidi.
Mara baada ya mazoezi ya leo kocha Brandts anasema
anashukuru programu yake inakwenda vizuri, wachezaji wote wanaendelea na
mazoezi na hakuna majeruhi hata mmoja tangu waanze maandilizi ya
mzunguko wa pili hivyo anaamini kikosi chake kinaendelea kuimarika
zaidi.
"Ukiwa na wachezaji wako wote wapo fit ni jambo jema, kwani
unapata fursa ya kutoa maelekezo kwa wakati mmoja, kuwatambua na
kuwasimamia jinsi wanavyoyashika na kuyatumia katika kujenga timu bora"
alisema Brandts
Young Africans
imekua ikiendelea na mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
ya Vodacom pamoja na mashindano ya klabu Bingwa Afrika ambayo
inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Februari 2014.
Timu
itaendelea kufanya mazoezi kila siku kulingana na programu ya mwalimu
mpaka wachezaji wengine waliopo na vikosi vya timu za Taifa katika
mashindano ya CECAFA Challenge nchini Kenya watakaporejea na kujumuika
na wenzao katika maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo wa "Nani Mtani
Jembe" .
No comments:
Post a Comment