Wanamichezo mashuhuri, duniani wametoa rambi rambi zao kwa hayati Nelson Mandela, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Akikaririwa bondia wa zamani wa uzito wa juu duniani Mohamed Ali amesema
"Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Pele anasema
"Mandela alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana maishani mwake. Ni shujaa wangu.’’
Mwanamasumbwi huyo aliongeza kusema kuwa, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa
mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi
pamoja chuki na uhasama.
Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''
" Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.’’
Tiger Woods naye ambaye ni mchezaji golfu mashuhuri zaidi duniani, alisema daima atamkumbuka Mandela.
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza,David Beckham akasema kuwa anamlilia sana Mandela na kuwa
yuko pamoja na familia yake.
''Tumepoteza mtu muhimu sana na shujaa
wetu,’’ Alisema Beckham.
Naye mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter , amesema kuwa anaomboleza sana na anahisi uchungu mwingi kufuatia kifo cha Mandela.
No comments:
Post a Comment