Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuwashinda mshambuliaji wa Barcelona Lionel
Messi na Franck Ribery wa Bayern Munich katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo wa Fifa ya Ballon
d'Or kwa mwaka 2013.
Nahodha huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 28, ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara ya kwanza mwaka 2008, alipigiwa kuara na makocha, manahodha na waandishi wa habari wa mchezo huo hii leo.
Mlinda mlango wa Ujerumani Nadine Angerer ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa tuzo za wanawake.
Kocha wa zamani wa Bayern Munich Jupp Heynckes amechukua nafasi ya kocha bora wa mwaka.
Messi mwenye umri wa miaka 26 alishinda tuzo hiyo mara nne mfululizo miaka minne iliyopita.
No comments:
Post a Comment