Lionel Messi amerejea nchini Hispania akitokea nyumbani kwao Argentina na ameaanza mazoezi na wenzake ndani ya kikosi cha Barcelona wakati akisubiri kauli ya daktari wa timu hiyo kaunza kucheza rasmi.
Messi alijitonesha msuli wa mguu wa kushoto Novemba 10 na amekuwa nyumbani kwao akiendelea kujiuguza tangu Novemba 29.
Barcelona pia imesema kuwa mlinda mlango Victor Valdes ameruhusiwa rasmi na daktari wa timu hiyo kuanza mazoezi.
Valdes anatarajiwa kuanza kudaka tika mchezo wa ligi kuu Jumapili katika uwanja wa nyumbani wa Nou Camp dhidi ya Elche kwa mara ya kwanza tangu aumie msuli wa mguu wa kulia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya Hispania dhidi ya Afrika kusini.
Barcelona inaongoza ligi ya Hispania ikiwa sambamba na Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment