Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameendelea kusisitiza kuwa vijana wake wameonesha ushahidi tosha kuwa wana nguvu na ari inayohitajika kunyakua taji
la Ligi ya Premier ya Uingereza msimu huu baada ya kungoja kwa muda
mrefu.
Ushindi wao wa bao 2-0 wa dakika za mwisho mwisho dhidi
ya Cardiff City Jumatano, umempa matumaini makubwa mzee Wenger ya kuwa Arsenal ni miongoni mwa wale
wanaogombania kikombe cha ubingwa walikishinda mara ya mwisho mwongo
mmoja uliopita.
Ingawa Manchester City na Chelsea wanamfuata katika msimamo wa ligi hiyo Arsenal wanazidi kuwapinga kujitutumua msimu huu na wakitaka wababe hao wasalimu
amri.
Nicklas Bendtner na Theo Walcott walikamilisha ushindi huo ikisalia
dakika chache kipenga cha mwisho kupulizwa na kuipa Arsenal uongozi wa msimamo.
“Kuna umoja dhabi kikosini. Wachezaji wananidhamu na hilo linaleta tofauti. Ikiwa hilo halipo mashindanoni, basi
hauna nafasi ya kutwaa ubingwa,” Wenger alisema.
Bendtner aliibuka shujaa kwenye mechi hiyo baada ya kufunga la kwanza
ikisalia dakika mbili baada ya Cardiff kumudu mashabulizi ya Arsenal
kwa kujenga mwamba kwenye ngome yao.
Raia huyo wa Denmark anazidi kuwashawishi wale ambao walikuwa
wamekata tamaa na uwezo wake wakati fulani, huku akiwakera mashabiki wa Arsenal.
“Ni mchezaji ambaye amepitia mengi magumu kwa hivyo, ningelitaka
kumsifu sana,” anasema Wenger, ambaye alitangaza kwamba mshambuliaji huyu
aliumiza kifundo cha mguu wakati akifunga bao lake.
“Nilimwambia kuwa amefikia kiwango nilichotaka awe na akiendelea kunawiri kwa njia hiyo, atarejea kwenye kikosi.
“Kwa bahati mbaya, alijeruhiwa na inaonekana atakosa mchezo wiki
kadhaa. Nina huzuni sana hususan kwake binafsi na timu yote kwa ujumla.”
No comments:
Post a Comment