Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa mshambuliaji wake Fernando Torres anakabiliwa na matatizo ya mguu ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima.
Maumivu ya mshambuliaji huyo yamekuja akitokea benchi katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 wa ligi kuu ya Premier dhidi ya Manchester United Jumapili iliyopita.
Hali hiyo itamlazimu Mourinho kusalia na washambuliaji Samuel Eto'o na Demba Ba katika kikosi cha kwanza lakini meneja huyo amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ndiye mchezaji pekee katika kikosi chake aliye majeruhi
No comments:
Post a Comment