KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, February 21, 2014

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA: BRAZIL BILA YA BIG MEN SAFU YA USHAMBULIAJI TATIZO KWA BIG PHIL WANAELEKEA VIPI KWENYE FAINALI?

Waswahili wanasema Kelele za chura hazimnyimi tembo kunywa maji. Haya ni maneno ambayo kwa wenyeji wa fainali za kombe dunia Brazil wamekuwa wakiyatumia.

Na kwasasa ikiwa ni miezi minne imesalia kabla ya ngarambe ya kombe la dunia haijaanza hali ya matayarisho bado inakabiliwa na tatizo moja kubwa.

Kubwa zaidi ni lile la kutokukamilika kwa viwanja pamoja na maandamano yasiyokwisha ya kupinga kuandaliwa kwa kombe la dunia nchini Brazil.

Kimsingi ni kwamba Brazil wanaendelea na maandalizi ya fainali hizo licha ya kukosolewa kwa kasoro kadhaa zilizojitokea na zinazo endelea kuonekana huku zikitafutiwa ufumbuzi.

Kwa upande wa maandaizi ya kikosi cha wenyeji hao wa fainali hizo, wanaonekana wakikabiliwa na tatizo la kutokuwa na mshambuliaji wa kati mwenye mwili na uwezo mkubwa.

Angalia, Luiz Felipe Scolari (Big Phil, akipanga safu na njia?) Anapenda kuwa na mtu mwenye mwili mkubwa. Mipango yake ni kuhakikisha kuwa wanashinda taji lakini atafanikiwa vipi bila ya kuwa Centre men mwenye umbile kubwa.
Little short up front: Big Phil (Felipe Scolari) lacks the big man up front he believes his Brazil team need
Kasoro kubwa safu ya ushambuliaji: Big Phil (Felipe Scolari) anakosa -big man up front- ana amini kikosi chake cha Brazil kinahitaji mtu wa aina hiyo
Injured: Scolari's first-choice 'big man', Fluminese's Fred, has struggled with goals and injury in recent months
Majeruhi: Chaguo la kwanza ni 'big man', Fred wa Fluminese amekuwa akikabiliwa na uhaba wa magoli na mejeruhi katika miezi ya karibuni.
Atletico Mineiro's Jo in action
Internacional forward Leandro Damiao playing for Brazil
Mbadala wa Fred  Jo (pichani juu kabisa) na Leandro Damiao wanatazamiwa kushirikiana na Neymar safu ya ushambuliaji
Bad press: Fred has irritated the Brazilian public by being photographed lounging on the beach while injured
Habari mbaya: Fred amewaumiza Wabrazil kwa kupigwa picha akiwa ufukweni katika kipindi cha majeraha yake.

 Scolari amekaririwa siku saba zilizopita wakati akitangaza kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika kusini.
'Nampenda mshambuliaji wa kati ambaye anatulia ndani ya eneo la hatari, ambaye ana nguvu anapokuwa ameruka hewani'

Mtu ambaye anatulia katika eneo la 18 ni Fred, mshambuliaji wa Fluminense ambaye kinsingi anapendwa sana na Scolari na amefunga magoli tisa katika michezo 10 ya kimataifa mwaka jana. 

Tatizo ni kwamba tangu alipofunga goli kwa mara ya mwisho mwezi Agosti, amekuwa akionekana akifanya matanuzi katika kipindi ambacho amekuwa majeruhi huko katika ufukwe wa Rio. 

Mbadala wa Fred ni Leandro Damiao au nyota wa Manchester City Jo ambaye hayuko vizuri, lakini wanaoneka kuleta matumaini kwa kufnga magoli nane na haijulikani ni nani atakaye kuwa pacha wa Neymar.
Marksman: Atletico Madrid's Diego Costa has pledged his future to Spain, much to Scolari's frustration
Pengine angekuwa ni mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa ambaye aliamua kuweka maisha yake ya soka la kimataifa nchini Hispania na kumchanganya Scolari

Wakati hali ikiwa hivyo jina ambalo limekuwa likitamkwa midomoni mwa kila mwenyekiti wa timu zilizo katika nafasi nne za juu katika ligi ya Premier nchini England ni Diego Costa.
 
Wakati Fred akikosa penati wikiendi hii huko Rio kwa upande wa Costa wa Atletico Madrid ameendeleza kasi yake ya ufungaji La Liga.

Baada ya kuchagua kuiwakilisha Hispania badala ya nchi aliyozaliwa maamuzi ambayo aliyafikia mwezi Oktoba, jina la Costa lilimchefua Big Phil.

No comments:

Post a Comment