Manchester United hatimaye imekubali kutoa kiasi cha pauni milioni £44 kwa mkataba wakudumu kwa ajili ya mshambuliaji Radamel Falcao.
United imekubali masharti ya klabu ya Monaco kuhusu Falcao ambaye alijiunga kwa mkopo wa muda mrefu uliokuwa na thamani ya pauni milion £6 usajili uliofanyika siku ya mwisho ya uhamisho wa kiangazi
Mabingwa mara 20 wa ligi ya England, United, wana uamuzi ndani ya makubaliano ya kimkataba kumsajili kama wataridhishwa na kiwango cha Falcao kutegemeana na afya yake wakati huo.
Falcao kwasasa anapokea mshahara wa pauni £240,000 kwa wiki na United imekubali kwa masharti yale yale kukamilisha mpango wa muda mrefu.
Wakala wa Falcao Jorge Mendes, amekuwa na ukaribu na watendaji wakuu wa United huku pia mshambuliaji mwenyewe akionyesha kutaka kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya msimu.
Ndani ya mkataba wa sasa wa mkopo wa baina ya United na Falcao, kuna kipengelea kinacho ipa fursa United kutathmini kiwango cha mchezaji huyo na hali ya afya kwa wakati huo kabla ya kuingia makubalino mengine, kufuatia Falcao kuwa katika maumivu ya mguu kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kiasi kusababisha mshambuliaji huyo kuikosa fainali ya kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment